Matumizi ya utanzia katika riwaya teule za Said Ahmed Mohamed

Loading...
Thumbnail Image
Date
2015
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Chuo Kikuu cha Dodoma
Abstract
Tasnifu hii, inahusu Matumizi ya Utanzia katika Riwaya Teule za Said Ahmed Mohamed. Riwaya zilizochuguzwa ni Utengano, Dunia Mti Mkavu na Kiza Katika Nuru. Dhana ya utanzia katika tasnifu hii ina maana ya maneno matendo au mazingira yanayozua kwa hadhira huzuni, jitimai, majonzi, masikitiko, majuto na maumivu ya mwili, roho au akili. Utanzia unajengwa na vipengele kama vile vifo, ajali, vifungo, mabalaa, ulemavu, vilio, maradhi, njaa na mateso. Yumkini, hakuna uchunguzi wa kutosha kuhusu matumizi ya utanzia katika kazi za fasihi ya Kiswahili. Hali hii imesababisha tatizo katika kuzielewa kazi mbalimbali za fasihi ya Kiswahili. Utafiti ulifanyika maktabani na uwandani. Maktabani tuliyadurusu mapitio mbalimbali kama vile: Majarida, tasnifu, tahakiki, makala na vitabu. Uwandani tulitumia mbinu ya mahojiano, majadiliano na udodosi. Kwa namna fulani mbinu hizi zilitusaidia katika kukusanya data mbalimbali zinazohusiana na utafiti huu. Maeneo ya Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Kusini Unguja, Dodoma na Dares Salaam yalitumika katika ukusanyaji wa data. Utafiti ulitumia nadharia ya Mwitiko wa Msomaji ambayo ilitumika kwa kupata fikra binafsi za wasomaji kutokana na uelewa wao wa vitabu teule walivyovisoma. Uchambuzi wa data uliegemea katika maelezo kwa kuwa utafiti huu ni wa kitaamuli. Hivyo, haukujihusisha na mwegamo wa kitakwimu. Matokeo ya utafiti yanaonyesha utanzia ni mbinu ya kibunulizi inayofungamana na utanzu mkongwe wa tamthiliya za kitanzia ambazo ndani yake hutoa athari maalum kwa wasomaji.
Description
Tasnifu (Shahada ya Uzamili ya Sayansi Jamii katika Fasihi ya Kiswahili)
Keywords
Utanzia, Riwaya, Said Ahmed Mohamed, Riwaya za Said Ahmed Mohamed, Utengano, Dunia Mti Mkavu, Kiza Katika Nuru, Fasihi ya Kiswahi
Citation
Ali, H. K. (2015). Matumizi ya utanzia katika riwaya teule za Said Ahmed Mohamed. Dodoma: Chuo Kikuu cha Dodoma