Matumizi ya utanzia katika riwaya teule za Said Ahmed Mohamed

dc.contributor.authorAli, Haji Khatibu
dc.date.accessioned2019-08-21T06:17:23Z
dc.date.available2019-08-21T06:17:23Z
dc.date.issued2015
dc.descriptionTasnifu (Shahada ya Uzamili ya Sayansi Jamii katika Fasihi ya Kiswahili)en_US
dc.description.abstractTasnifu hii, inahusu Matumizi ya Utanzia katika Riwaya Teule za Said Ahmed Mohamed. Riwaya zilizochuguzwa ni Utengano, Dunia Mti Mkavu na Kiza Katika Nuru. Dhana ya utanzia katika tasnifu hii ina maana ya maneno matendo au mazingira yanayozua kwa hadhira huzuni, jitimai, majonzi, masikitiko, majuto na maumivu ya mwili, roho au akili. Utanzia unajengwa na vipengele kama vile vifo, ajali, vifungo, mabalaa, ulemavu, vilio, maradhi, njaa na mateso. Yumkini, hakuna uchunguzi wa kutosha kuhusu matumizi ya utanzia katika kazi za fasihi ya Kiswahili. Hali hii imesababisha tatizo katika kuzielewa kazi mbalimbali za fasihi ya Kiswahili. Utafiti ulifanyika maktabani na uwandani. Maktabani tuliyadurusu mapitio mbalimbali kama vile: Majarida, tasnifu, tahakiki, makala na vitabu. Uwandani tulitumia mbinu ya mahojiano, majadiliano na udodosi. Kwa namna fulani mbinu hizi zilitusaidia katika kukusanya data mbalimbali zinazohusiana na utafiti huu. Maeneo ya Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Kusini Unguja, Dodoma na Dares Salaam yalitumika katika ukusanyaji wa data. Utafiti ulitumia nadharia ya Mwitiko wa Msomaji ambayo ilitumika kwa kupata fikra binafsi za wasomaji kutokana na uelewa wao wa vitabu teule walivyovisoma. Uchambuzi wa data uliegemea katika maelezo kwa kuwa utafiti huu ni wa kitaamuli. Hivyo, haukujihusisha na mwegamo wa kitakwimu. Matokeo ya utafiti yanaonyesha utanzia ni mbinu ya kibunulizi inayofungamana na utanzu mkongwe wa tamthiliya za kitanzia ambazo ndani yake hutoa athari maalum kwa wasomaji.en_US
dc.identifier.citationAli, H. K. (2015). Matumizi ya utanzia katika riwaya teule za Said Ahmed Mohamed. Dodoma: Chuo Kikuu cha Dodomaen_US
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/20.500.12661/1026
dc.language.isoKiswen_US
dc.publisherChuo Kikuu cha Dodomaen_US
dc.subjectUtanziaen_US
dc.subjectRiwayaen_US
dc.subjectSaid Ahmed Mohameden_US
dc.subjectRiwaya za Said Ahmed Mohameden_US
dc.subjectUtenganoen_US
dc.subjectDunia Mti Mkavuen_US
dc.subjectKiza Katika Nuruen_US
dc.subjectFasihi ya Kiswahien_US
dc.titleMatumizi ya utanzia katika riwaya teule za Said Ahmed Mohameden_US
dc.typeDissertationen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
HAJI KHATIBU ALI.pdf
Size:
1.58 MB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: