Matamshi na tahajia ya istilahi mkopo za Kiingereza katika Kiswahili: Mifano kutoka istilahi za sayansi ikisiri
Loading...
Date
2022
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
The University of Dar es Salaam
Abstract
Lengo la makala haya ni kuonesha ruwaza ya matamshi na tahajia ya Istilahi Mkopo (kuanzia sasa IM) za Kiingereza zinazoingizwa katika Kiswahili. Mtazamo wa asasi zinazohusika na uundaji istilahi kama vile Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA) na Taasisi ya Taaluma za Kiswahili (TATAKI) kuhusu matamshi na tahajia ya IM unaonesha kuwa IM zenye matamshi kama yalivyo katika Kiswahili na kuwa na tahajia ya IM zenye muundo wa maandishi kama ilivyo katika Kiingereza. Data na hoja zilizowasilishwa katika makala hii zimetokana na hojaji, usaili na upitiaji nyaraka[1]. Hivyo, data hizo zinadhihirisha kuwa kuna uhalali wa kuangalia upya ruwaza ya matamshi na tahajia ya IM za Kiingereza katika Kiswahili. Makala haya yanabainisha kuwa IM ziwe na ruwaza ya matamshi kama ilivyo katika Kiingereza. Kwa mfano, <hydrogen> - /haidrojeni/ na tahajia iwe ni ile ya muundo wa matamshi badala ya ule wa maandishi. Kwa mfano, <hydrogen>- <haidrojeni> *<hidrojeni>. Makala yanatoa mwongozo wa matamshi na tahajia ya IM katika Kiswahili.
Description
Abstract. Full text article available at https://journals.udsm.ac.tz/index.php/kiswahili/article/view/4749
Keywords
Matamshi, Istilahi mkopo, Istilahi za sayansi, Baraza la Kiswahili Tanzania, BAKITA, TATAKI, Taasisi ya Taaluma za Kiswahili, IM
Citation
Philipo, Z. T. (2022). Matamshi na Tahajia ya Istilahi Mkopo za Kiingereza katika Kiswahili Mifano kutoka Istilahi za Sayansi Ikisiri. Kiswahili, 84(1).