Matumizi ya ujaala katika ushairi wa Kiswahili: ulinganisho wa diwani za Mathias Mnyampala na Amri Abedi Kaluta
Loading...
Date
2017
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Chuo Kikuu cha Dodoma
Abstract
Utafiti huu unahusu matumizi ya ujaala katika ushairi wa Kiswahili: Ulinganisho wa diwani za Mathias Mnyampala na Amri Abedi Kaluta. Ujaala ni falsafa ambayo hutawala na kuongoza maisha ya binadamu (Ponera, 2014). Falsafa ya ujaala katika ushairi wa Kiswahili haijatafitiwa vya kutosha hivyo, kuwanyima fursa wasomaji na watunzi wa kazi za fasihi na kutoelewa dhana ya ujaala. Hii imemsukuma mtafiti kuchunguza matumizi ya falsafa ya ujaala katika ushairi wa Kiswahili.
Kwa kiasi kikubwa, utafiti huu ulifanyika maktabani, baadaye mtafiti alienda uwandani kufanya mahojiano na wataalamu pamoja na familia za waandishi teule. Kwa mintarafu hiyo, mkabala wa kitaamuli ndio uliotumika katika uwasilishaji wa data za utafiti huu. Uchanganuzi wa data ulitumia nadharia ya udhanaishi kutokana na kuakisi kwake suala la kuamini katika uwepo wa Mungu kama inavyojidhihirisha katika diwani za waandishi teule zilizotumika katika utafiti huu.
Matokeo ya utafiti huu yamebaini kuwa, katika ushairi wa Kiswahili kuna matumizi makubwa ya falsafa ya ujaala. Matumizi hayo hufanana na kutofautiana miongoni mwa waandishi teule waliotumika katika kazi hii. Kuna mpishano mkubwa baina ya jamii moja na nyingine. Licha ya mpishano huo, wote huamini katika kani ya Mungu inayotawala na kuongoza maisha ya binadamu. Utatifi huu uliibua michango mipya mbalimbali. Utafiti huu umependekeza tafiti zaidi zifanyike juu ya matumizi ya ujaala katika riwaya na tamthilia.
Description
Shahada ya Uzamili katika Fasihi ya Kiswahili
Keywords
Ushairi, Ujaala, Ulinganifu, Ufananishi, Mathias Mnyampala, Amri Abedi Kaluta, Kiswahili, Falsafa, Falsafa ya ujaala, Matumizi ya ujaala, Diwani, Ushairi wa Kiswahili
Citation
Mbwambo, G. (2017). Matumizi ya ujaala katika ushairi wa Kiswahili: ulinganisho wa diwani za Mathias Mnyampala na Amri Abedi Kaluta. Dodoma: Chuo Kikuu cha Dodoma