Matumizi ya ujaala katika ushairi wa Kiswahili: ulinganisho wa diwani za Mathias Mnyampala na Amri Abedi Kaluta

dc.contributor.authorMbwambo, Grace
dc.date.accessioned2018-10-09T08:18:17Z
dc.date.available2018-10-09T08:18:17Z
dc.date.issued2017
dc.descriptionShahada ya Uzamili katika Fasihi ya Kiswahilien_US
dc.description.abstractUtafiti huu unahusu matumizi ya ujaala katika ushairi wa Kiswahili: Ulinganisho wa diwani za Mathias Mnyampala na Amri Abedi Kaluta. Ujaala ni falsafa ambayo hutawala na kuongoza maisha ya binadamu (Ponera, 2014). Falsafa ya ujaala katika ushairi wa Kiswahili haijatafitiwa vya kutosha hivyo, kuwanyima fursa wasomaji na watunzi wa kazi za fasihi na kutoelewa dhana ya ujaala. Hii imemsukuma mtafiti kuchunguza matumizi ya falsafa ya ujaala katika ushairi wa Kiswahili. Kwa kiasi kikubwa, utafiti huu ulifanyika maktabani, baadaye mtafiti alienda uwandani kufanya mahojiano na wataalamu pamoja na familia za waandishi teule. Kwa mintarafu hiyo, mkabala wa kitaamuli ndio uliotumika katika uwasilishaji wa data za utafiti huu. Uchanganuzi wa data ulitumia nadharia ya udhanaishi kutokana na kuakisi kwake suala la kuamini katika uwepo wa Mungu kama inavyojidhihirisha katika diwani za waandishi teule zilizotumika katika utafiti huu. Matokeo ya utafiti huu yamebaini kuwa, katika ushairi wa Kiswahili kuna matumizi makubwa ya falsafa ya ujaala. Matumizi hayo hufanana na kutofautiana miongoni mwa waandishi teule waliotumika katika kazi hii. Kuna mpishano mkubwa baina ya jamii moja na nyingine. Licha ya mpishano huo, wote huamini katika kani ya Mungu inayotawala na kuongoza maisha ya binadamu. Utatifi huu uliibua michango mipya mbalimbali. Utafiti huu umependekeza tafiti zaidi zifanyike juu ya matumizi ya ujaala katika riwaya na tamthilia.en_US
dc.identifier.citationMbwambo, G. (2017). Matumizi ya ujaala katika ushairi wa Kiswahili: ulinganisho wa diwani za Mathias Mnyampala na Amri Abedi Kaluta. Dodoma: Chuo Kikuu cha Dodomaen_US
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/20.500.12661/456
dc.language.isoKiswen_US
dc.publisherChuo Kikuu cha Dodomaen_US
dc.subjectUshairien_US
dc.subjectUjaalaen_US
dc.subjectUlinganifuen_US
dc.subjectUfananishien_US
dc.subjectMathias Mnyampalaen_US
dc.subjectAmri Abedi Kalutaen_US
dc.subjectKiswahilien_US
dc.subjectFalsafaen_US
dc.subjectFalsafa ya ujaalaen_US
dc.subjectMatumizi ya ujaalaen_US
dc.subjectDiwanien_US
dc.subjectUshairi wa Kiswahilien_US
dc.titleMatumizi ya ujaala katika ushairi wa Kiswahili: ulinganisho wa diwani za Mathias Mnyampala na Amri Abedi Kalutaen_US
dc.typeDissertationen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
GRACE MBWAMBO- RIPOTI.pdf
Size:
1.15 MB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: