Usawiri wa mwanamke katika tamthiliya teule za Penina Muhando

dc.contributor.authorGeorge, Grace
dc.date.accessioned2020-03-05T07:37:07Z
dc.date.available2020-03-05T07:37:07Z
dc.date.issued2014
dc.descriptionTasnifu (MA Kiswahili)en_US
dc.description.abstractUtafiti huu umejadili kuhusu Usawiri wa Mwanamke katika Tamthiliya Teule za Penina Mhando. Tatizo lililojenga utafiti huu ni kutokana na hali ya kila siku ya waandishi wa tamthiliya za Kiswahili wakiwemo wanaume, kumkweza mwanaume kinafasi na kimajukumu na kumshusha mwanamke, hivyo utafiti huu ulijikita kuchunguza nafasi ya mwanamke katika tamthilia teule za Penina Muhando. Utafiti huu ulitumia mbinu ya maktabani kwa kuchunguza kazi mbalimbali ili kupata ruwaza ya jumla kuhusu nafasi ya mwanamke na mgawanyo wa majukumu kijinsia, pia vitabu teule ambavyo ni Hatia (1972) na Nguzo Mama (1982) vimesomwa na kuchunguzwa kwa makini na kuona jinsi mwanamke alivyochorwa. Mahojiano yalifanyika ili kupata mawazo mbalimbali kuhusu mada ya utafiti. Pia umeongozwa na nadharia ya Ufeministi. Hivyo utafiti huu umebaini kuwa kuna tofauti kubwa za kimajukumu kati ya mwanaume na mwanamke. Kwa upande mmoja mwanamke amechorwa kwa mtazamo hasi na chanya yaani ameonekana ni kiumbe duni, mnyonge, na hivyo kuendelea kumdharau, kumkejeli na kumdhihaki. Kwa upande mwingine mwanamke amechorwa kama mshauri, mlezi, mbunifu, mvumilivu na mtu mwenye huruma na ushirikiano katika jamii. Pia utafiti huu umebaini kuwa zipo athari mbalimbali zinazosababishwa na uchorwaji wa mwanamke katika tamthilia. Athari mojawapo ni kuigwa kwa matendo machafu ambayo yanasababisha kudharaulika na kuendelea kukandamizwa kwa wanawake. Hivyo basi kutokana na matokeo ya utafiti huu tumefikia mahitimisho kuwa katika jamii nafasi ya mwanamke na mgawawanyo wa majukumu huwa tofauti na mwanaume kwa sababu ya mila na tamaduni mbovu ambazo humchukulia mwanamke kama kiumbe duni wakati wote ingawa uhalisia wa sasa hauko hivyo.en_US
dc.identifier.citationGeorge, G. (2014). Usawiri wa mwanamke katika tamthiliya teule za Penina Muhando (Tasnifu). Chuo Kikuu cha Dodoma, Dodoma.en_US
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/20.500.12661/1990
dc.language.isoenen_US
dc.publisherChuo Kikuu cha Dodomaen_US
dc.subjectKiswahilien_US
dc.subjectJinsiaen_US
dc.subjectHatien_US
dc.subjectNguzo mamaen_US
dc.subjectMajukumuen_US
dc.subjectUnyongeen_US
dc.subjectMilaen_US
dc.subjectTamadunien_US
dc.subjectUsawiri mwanamkeen_US
dc.subjectUsawiri mwanaumeen_US
dc.subjectTamthiliyaen_US
dc.subjectTamthiliya kiswahilien_US
dc.subjectPenina Mhandoen_US
dc.subjectNadharia ufeministien_US
dc.titleUsawiri wa mwanamke katika tamthiliya teule za Penina Muhandoen_US
dc.typeDissertationen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Grace George.pdf
Size:
882.15 KB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: