Athari za kimaendeleo katika muktadha wa nyimbo za ngoma ya mbassa ya jamii ya Wachagga
Loading...
Date
2012
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Chuo kikuu cha Dodoma
Abstract
Utafiti huu ulilenga kuchunguza athari za kimaendeleo katika muktadha wa nyimbo za ngoma ya Mbassa. Nyimbo za ngoma ya Mbasssa zilikuwa zinaimbwa katika muktadha wa unyago. Kwa sasa nyimbo hizi haziimbwi katika muktadha wa unyago kutokana na mabadiliko ya kimaendeleo, yakiwemo masuala ya utandawazi, mabadiliko ya sayansi na teknolojia, kupanuka kwa kiwango cha elimu, kubadilika kwa mfumo wa siasa, masuala ya kibiashara na mwingiliano katika tamaduni, kumeathiri nyimbo za ngoma ya Mbassa. Nyimbo hizi bado zipo na zinaimbwa katika miktadha ya sherehe za harusi, sherehe za kidini na kwenye kampeni za kisiasa. Nadharia iliyotumika katika utafiti huu ni ya Kihemenitiki. Nadharia hii inatizama maana ya fasihi, namna fasihi inavyohusiana na kusudi la mwandishi, na kama inakuwa rahisi kupata uelewaji wa ndani wa kazi ya fasihi kutegemeana na mazingira na historia ya hadhira inayohusika. Nadharia hii imesaidia kubaini na kuchambua mada ya utafiti ambayo inahusiana na athari za kimaendeleo katika muktadha wa nyimbo za ngoma ya Mbassa. Utafiti huu ulitumia mbinu mbalimbali zikiwemo mbinu ya udadisi, mbinu ya kusogezeana, mbinu ya uchaguzi holela, mbinu ya ufafanuzi wa matini pia ilitumika mbinu ya mchakato wa ukusanyaji data na udhibiti wake. Matokeo ya utafiti yalizingatia suala la kimuktadha katika kuchambua maudhui ya ngoma ya Mbassa, kujua namna maudhui hayo yanayosawiri katika jamii ya sasa. Pia matokeo ya utafiti yalitizama namna nyimbo za ngoma ya Mbassa zinazoimbwa wakati huu kama zinaendana au zinasawiri mabadiliko ya kimaendeleo katika jamii.
Description
Dissertation (Shahada Uzamili Fasihi ya Kiswahili)
Keywords
Wachagga, Nyimbo, Ngoma, Mbassa, Unyago, Sherehe, Fasihi
Citation
Mboya, K. A. (2012). Athari za kimaendeleo katika muktadha wa nyimbo za ngoma ya mbassa ya jamii ya Wachagga. Dodoma: Chuo kikuu cha Dodoma