Athari za kimaendeleo katika muktadha wa nyimbo za ngoma ya mbassa ya jamii ya Wachagga

dc.contributor.authorMboya, Kolman A.
dc.date.accessioned2019-09-05T11:26:44Z
dc.date.available2019-09-05T11:26:44Z
dc.date.issued2012
dc.descriptionDissertation (Shahada Uzamili Fasihi ya Kiswahili)en_US
dc.description.abstractUtafiti huu ulilenga kuchunguza athari za kimaendeleo katika muktadha wa nyimbo za ngoma ya Mbassa. Nyimbo za ngoma ya Mbasssa zilikuwa zinaimbwa katika muktadha wa unyago. Kwa sasa nyimbo hizi haziimbwi katika muktadha wa unyago kutokana na mabadiliko ya kimaendeleo, yakiwemo masuala ya utandawazi, mabadiliko ya sayansi na teknolojia, kupanuka kwa kiwango cha elimu, kubadilika kwa mfumo wa siasa, masuala ya kibiashara na mwingiliano katika tamaduni, kumeathiri nyimbo za ngoma ya Mbassa. Nyimbo hizi bado zipo na zinaimbwa katika miktadha ya sherehe za harusi, sherehe za kidini na kwenye kampeni za kisiasa. Nadharia iliyotumika katika utafiti huu ni ya Kihemenitiki. Nadharia hii inatizama maana ya fasihi, namna fasihi inavyohusiana na kusudi la mwandishi, na kama inakuwa rahisi kupata uelewaji wa ndani wa kazi ya fasihi kutegemeana na mazingira na historia ya hadhira inayohusika. Nadharia hii imesaidia kubaini na kuchambua mada ya utafiti ambayo inahusiana na athari za kimaendeleo katika muktadha wa nyimbo za ngoma ya Mbassa. Utafiti huu ulitumia mbinu mbalimbali zikiwemo mbinu ya udadisi, mbinu ya kusogezeana, mbinu ya uchaguzi holela, mbinu ya ufafanuzi wa matini pia ilitumika mbinu ya mchakato wa ukusanyaji data na udhibiti wake. Matokeo ya utafiti yalizingatia suala la kimuktadha katika kuchambua maudhui ya ngoma ya Mbassa, kujua namna maudhui hayo yanayosawiri katika jamii ya sasa. Pia matokeo ya utafiti yalitizama namna nyimbo za ngoma ya Mbassa zinazoimbwa wakati huu kama zinaendana au zinasawiri mabadiliko ya kimaendeleo katika jamii.en_US
dc.identifier.citationMboya, K. A. (2012). Athari za kimaendeleo katika muktadha wa nyimbo za ngoma ya mbassa ya jamii ya Wachagga. Dodoma: Chuo kikuu cha Dodomaen_US
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/20.500.12661/1744
dc.publisherChuo kikuu cha Dodomaen_US
dc.subjectWachaggaen_US
dc.subjectNyimboen_US
dc.subjectNgomaen_US
dc.subjectMbassaen_US
dc.subjectUnyagoen_US
dc.subjectShereheen_US
dc.subjectFasihien_US
dc.titleAthari za kimaendeleo katika muktadha wa nyimbo za ngoma ya mbassa ya jamii ya Wachaggaen_US
dc.typeDissertationen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Kolman Aloyce Mboya.pdf
Size:
1.49 MB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: