Hali ya kupendwa kwa nyimbo za injili kama fasihi pendwa: mfano nyimbo za Christina Shusho
Loading...
Date
2017
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Chuo Kikuu cha Dodoma
Abstract
Utafiti huu unahusu misingi ya kupendwa kwa nyimbo za Injili kama fasihi pendwa kwa kuangalia nyimbo za Christina Shusho. Nyimbo za Injili ni mpangilio wa sauti za kuimbwa sambamba na vitendo katika uhalisia wake ukipambanuliwa kwa gitaa na zumari wenye muonekano wa kanisa, kwa maana maudhui yake huwa tofauti na miziki mingine na ni nyimbo zinazoelezea habari njema za Yesu Kristo. Fasihi pendwa ni fasihi ambayo inapendwa na watu wengi na inaleta mvuto kwa watu wengi na inatofautiana na tanzu nyingine za fasihi. Katika kufanikisha malengo ya utafiti, nadharia ya upokezi imetumika katika uchanganuzi wa data. Data ilikusanywa kutoka mikoa ya Dodoma na Dar es Salaam. Mbinu za usaili, ushuhudiaji, udurusu wa maandiko na majadiliano zilitumika katika kukusanya data, sambamba na matumizi ya kanda zilizorekodiwa wakati mtafiti akiwa uwandani. Utafiti umebaini kuwa nyimbo za Injili ni utanzu mmojawapo wa fasihi pendwa katika tanzu za fasihi za Kiswahili. Tumeona kuwa nyimbo za Injili ni nyimbo zenye wapenzi wengi. hii hutokana na namna mwimbaji anavyoimba, haiba yake na uwasilishaji wake na maudhui mbalimbali yanayojitokeza katika nyimbo za mwimbaji yanayoigusa jamii. Nyimbo za Injili kama utanzu mmojawapo wa fasihi simulizi ina mchango mkubwa katika kusana kazi za kifasihi na zina maudhui mbalimballi yanayoigusa jamii. Misingi ya kupendwa kwa nyimbo za Injili ni kitu amabacho kinahitaji tafiti zaidi za kitaaluma kutokana na umuhimu wake katika jamii. Inapendekezwa kuwa tafiti zifanywe katika tanzu nyingine za fasihi.
Description
Shahada ya Uzamili katika Fasihi ya Kiswahili
Keywords
Fasihi, Fasihi pendwa, Nyimbo, Nyimbo za injili, Christina Shusho, Tanzu za fasihi, Nadharia, Nadharia ya upokezi, Dodoma, Dar es Salaam, Fasihi ya Kiswahili, Fasihi simulizi, Tanzania, Injili
Citation
Bitababaje, H. W. (2017). Hali ya kupendwa kwa nyimbo za injili kama fasihi pendwa: mfano nyimbo za Christina Shusho. Dodoma: Chuo Kikuu cha Dodoma