Semi zilizoandikwa katika maeneo ya biashara: uchunguzi kuhusu asili, muundo, miktadha ya utokeaji na dhima

dc.contributor.authorShayo, Inocent Faustine
dc.date.accessioned2019-08-20T07:24:50Z
dc.date.available2019-08-20T07:24:50Z
dc.date.issued2015
dc.descriptionTasnifu (Shahada ya Uzamili katika Fasihi ya Kiswahili)en_US
dc.description.abstractTasnifu hii inatokana na utafiti uliofanywa kuhusu semi zilizoandikwa katika maeneo mbalimbali ya biashara. Mambo ya msingi yaliyochunguzwa katika semi hizi ni asili, miktadha ya utokeaji, miundo na dhima. Utafiti huu ulifanyika katika mji wa Same mkoani Kilimanjaro. Semi za biashara ni semi ambazo hujitokeza katika muktadha wa kibiashara kwa kuandikwa au kutumiwa katika mazungumzo ya kila siku ya kibiashara japokuwa utafiti uliangalia semi zilizoandikwa tu. Malengo mahususi ambayo yameuongoza utafiti huu yalikua manne ambayo ni: kubainisha semi mbalimbali zilizoandikwa katika maeneo ya biashara, kuchunguza miundo ya semi zilizoandikwa katika maeneo ya biashara, kuchunguza miktadha inayohusiana na kuibuka kwa semi zilizoandikwa katika maeneo ya biashara, pamoja na kuchunguza dhima za semi zilizoandikwa katika maeneo ya biashara. Nadharia ya Mwitikio wa msomaji ndiyo iliyotumika kuuongoza utafiti huu. Nadharia hii imetumika kwa sababu inahimiza juu ya mchango wa msomaji, mtazamaji au mwonaji wa kazi ya fasihi na sio mwandishi. Wauzaji, wamiliki na wateja wa maeneo mbalimbali ya biashara walihojiwa na kutoa maoni yao juu ya dhima na asili ya semi hizo. Hivyo, ili kufikia malengo ya utafiti huu nadharia hii ndiyo inayokidhi haja. Mbinu zilizotumika katika ukusanyaji wa data katika utafiti huu ni ushuhudiaji, udodosaji na maktabani. Vifaa vilivyotumika katika ukusanyaji wa data ni hojaji, kamera, ngamizi (kompyuta), shajara na simu. Utafiti umebaini kuwa semi zilizoandikwa katika maeneo mbalimbali ya biashara zimebeba dhima kubwa ambazo huielezea jamii katika nyanja zote yaani kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni. Vilevile, semi hizi huwa na miundo mbalimbali na hazitegemei muundo mmoja katika uandikwaji wake. Aidha, semi hizi hujitokeza katika miktadha tofauti tofauti kutegemeana na kusudio au dhima iliyobebwa. Utafiti huu umesaidia kuonesha na kutambulisha faida, umuhimu, na nafasi ya semi ambazo huandikwa katika maeneo ya biashara.en_US
dc.identifier.citationShayo, I. F. (2015). Semi zilizoandikwa katika maeneo ya biashara: uchunguzi kuhusu asili, muundo, miktadha ya utokeaji na dhima. Dodoma: Chuo Kikuu cha Dodomaen_US
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/20.500.12661/983
dc.language.isoKiswen_US
dc.publisherChuo Kikuu cha Dodomaen_US
dc.subjectSemien_US
dc.subjectBiasharaen_US
dc.subjectAsilien_US
dc.subjectMuundoen_US
dc.subjectMiktadhaen_US
dc.subjectDhimaen_US
dc.subjectDhima za semien_US
dc.subjectSameen_US
dc.subjectKilimanjaroen_US
dc.titleSemi zilizoandikwa katika maeneo ya biashara: uchunguzi kuhusu asili, muundo, miktadha ya utokeaji na dhimaen_US
dc.typeDissertationen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
INOCENT FAUSTINE SHAYO.pdf
Size:
1.99 MB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: